NEWS

Monday 19 September 2022

Madereva wa magari, bodaboda waishukuru Barrick kuwaboreshea barabara Nyamongo


Katapila la Barrick North Mara likikarabati barabara ya Nyamongo-Kewanja-Nyamwaga, Jumamosi iliyopita.

Na Mwandishi Wetu, Tarime
--------------------------------------

VIONGOZI wa vijiji na wananchi mbalimbali wameushukuru Mgodi wa Dhahabu wa North Mara chini ya Kampuni ya Barrick, kwa kuboresha barabara ya Nyamongo-Kewanja-Nyamwaga.

Barrick North Mara imekubali ombi kufanya maboresho ya barabara hiyo baada ya kuombwa na viongozi, wakiwemo wenyeviti wa vijiji vilivyo jirani na mgodi huo wilayani Tarime.

Wakizungumza na Sauti ya Mara wakati uboreshaji wa barabara hiyo ukiendelea Jumamosi iliyopita, wenyeviti wa serikali za vijiji hivyo walisema ilikuwa imeharibika na kusababisha usumbufu kwa watumiaji.

“Tunaishuku Kampuni ya Barrick North Mara kwa msaada huu wa kukarabti barabara hii kwa sababu ilikuwa imeharibika na kuwa kero kubwa kwa wananchi tunaoitumia.

“Hii siyo mara ya kwanza kwa mgodi huu kukarabati barabara zetu, hivi karibuni tulimuomba Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara wakatukarabatia barabara ya Kwinogo-Uwanja wa Ndege, tunashukuru sana,” alisema Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kewanja, Bunini John Bunini.

Kwa mujibu wa Bunini, misaada ya kijmii inyotolewa na kampuni hiyo ukiwemo huo wa kukarabati barabara, ina mchango mkubwa katika kuboresha mahusiano baina mgodi wa North Mara na wakazi wa vijiji vinavyouzunguka.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyakunguru, Chacha Makuri Gotono alisema “Ninatoa shukurani za dhati kwa Kampuni ya Barrick kwa kukubali ombi la kutuboreshea barabara hii, ninaomba mahusiano haya yaendelee kwa maendeleo ya wananchi katika ukanda huu wa machimbo ya madini.”

Nao madereva, makondakta na abiria wa magari yanayotumia barabara hiyo wameishukuru Kampuni ya Barrick North Mara wakisema ukarabati huo umewaondolea adha iliyokuwepo.

“Kwa kweli sisi madereva wa magari tunaotumia barabara hii kujitafutia riziki tunaishukuru sana Barrick kwa msaada huu wa kutuchongea barabara hii.

“Sasa hivi kama unavyoona barabara imesawazishwa, mabonde yaliyokuwa yamesababishwa na mvua hayapo tena, tunapita vizuri na hakuna malalamiko ya kuchelewesha abiria,” alisema Eric Mahiri anayeendesha gari linalofanya safari kati ya Tarime, Nyamwaga na Nyamongo.

Kwa upande wake, Zabron Mwita ambaye ni mwendesha pikipiki ya abiria (bodaboda) alisema “Tunaomba mtufikishie shukurani zetu kwa uongozi wa mgodi wa North Mara kwa kutuboreshea barabara hii, tumefurahi sana, sasa hivi tunapita bila kikwazo.”

Naye mkazi wa kijiji cha Kewanja, Brigitha Michael aliishukuru Barrick North Mara akisema uboreshaji wa barabara hiyo umewarahisishia hata wanawake usafiri wa kwenda kupata huduma mbalimbali, zikiwemo za afya.

“Tunaushukuru sana mgodi wa North Mara kwa kukarabtia barabara ya Nyamongo-Kewanja-Nyamwaga, hakika kitendo hiki kinadhihirisha jinsi wanavyojali wananchi wa vijiji vinavyopakana nao, tunashukuru sana,” alisema mwanakijiji huyo.
Barabara hii pia hutumiwa na magari ya watalii kwenda na kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Chanzo: Sauti ya Mara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages