NEWS

Wednesday 12 October 2022

Nyambari Nyangwine akabidhi msaada wa vitabu vya milioni 3 kwa Tarime Girls


Mdau wa maendeleo kwa muda mrefu, Nyambari Nyangwine, leo Oktoba 12, 2022 amekabidhi msaada wa vitabu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Tarime "Tarime Girls". Msaada huo umekabidhiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mara Online, Mugini Jacob (katikati pichani juu) kwa niaba ya Nyangwine, ambapo aliyeupokea ni Hezbon Peter Mwera, Mkurugenzi wa Professor Mwera Foundation (PMF) inayomiliki shule hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Tarime Girls, Mwalimu Maria Daniel Tarimo.

CEO wa Mara Online, Mugini Jacob, Mkurugenzi wa Taasisi ya PMF, Hezbon Mwera, walimu, viongozi mbalimbali na wanafunzi wa Tarime Girls wakionesha baadhi ya vitabu vya kiada na ziada vyenye thamani ya shilingi milioni tatu - vilivyotolewa msaada na mdau wa maendeleo, Nyambari Nyangwine, muda mfupi baada ya Jacob kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Nyangwine shuleni hapo, leo Oktoba 12, 2022. (Picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages