NEWS

Friday 14 October 2022

Mashirika ya Right to Play, AICT yakemea ukeketaji yakihamasisha haki ya mtoto wa kike



Na Mara Online News
-------------------------------

SHIRIKA la Right to Play kwa kushirikiana na AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe, yamehamasisha kabila la Wakurya kuachana na mila ya kukeketa mtoto wa kike, badala yake limwezeshe kupata haki sawa na mtoto wa kiume, ikiwemo elimu.

Hayo yalielezwa jana Oktoba 13, 2022 wakati wa madhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike kupitia tamasha maalumu la michezo, lililoandaliwa na mashirika hayo kwa wanafunzi wa shule za msingi Kimusi na Nyamiri zilizopo kata ya Nyamwaga wilayani Tarime, Mara.

“Wakurya tunapaswa kubadilisha mitazamo yetu, mila ya ukeketaji imepitwa na wakati na inachangia mimba za utotoni. Tunahitaji mtoto wa kike apewe haki sawa kama wa kiume,” alisisitiza Afisa Elimu Kata ya Nyansincha, Mwalimu Sophia Range (katikati pichani juu) aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo.

Mwalimu Range aliyashukuru mashirika ya Right to Play na AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe kuendeleza matamasha ya michezo kwa ajili ya kuhamasisha haki ya mtoto wa kike, akisema yamesaidia pia kupunguza utoro kwa wanafunzi wa shule za msingi katika eneo la mradi huo, yaani kata za Nyamwaga, Nyansincha na Itiryo wilayani Tarime.

Aidha, alisema mtoto wa kike kupungiziwa kazi za nyumbani kama kupika na kulea watoto, ili apate muda wa kujisomea kama ilivyo kwa mtoto wa kiume.

Tamasha hilo la michezo lilihitimishwa kwa washindi wa michezo ya mbalimbali kutoka Shule ya Msingi Kimusi kupewa zawadi.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike mwaka huu ni “Haki yetu ni Hatima yetu, Wakati ni sasa”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages