NEWS

Monday 3 October 2022

NMB Tarime, Sirari yaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kishindo



Na Mara Online News
-------------------------------

BENKI ya NMB Tawi la Tarime mkoani Mara, mapema leo Oktoba 3, 2022 asubuhi, imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja - kwa kuzungumza, kisha kukata keki na kupata chai maalumu pamoja na baadhi ya wateja wake.

“Leo tunayo furaha kuungana na dunia nzima kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, inayoadhimishwa wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka, na mwaka huu ni kuanzia Oktoba 3 hadi 7. Kaulimbiu ya maadhimisho haya mwaka huu ni ‘Sherehekea Huduma (Celebrate Service),” Meneja wa NMB Tawi la Tarime, Victorine Kimario amesema katika hafla hiyo.


Kimario amesema Benki hiyo inatumia maadhimisho hayo ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kutangaza maboresho katika huduma zake mbili zilizomo kwenye NMB Mkononi, yaani Mshiko Fasta na Spend to Save.

Amefafanua kuwa Spend to Save ni huduma inayomsaidia mteja kujiwekea akiba kulingana na matumizi yake, tofauti na awali ambapo mteja alitakiwa kwenda kujisajili kwenye ATM ya NMB ili aweze kuanza kujiwekea akiba kulingna na asilimia aliyoweka.

“Kuanzia sasa, tumeboresha huduma hii na sasa itapatikana kwenye NMB Mkononi, ambapo mteja ataweza kujisajili, kuangalia salio lake na hata kutoa fedha yake anapohitaji,” amesema Kimario.

Kuhusu Mshiko Fasta, amesema ni huduma inayompa mteja fursa ya kukopa fedha kupitia simu ya mkononi bila dhamana wala kufika matawini.

“Huduma hii inamwezesha mteja kukopa kuanzia shilingi 1,000 hadi 500,000 na kurejesha kati ya siku moja mpaka siku 28,” ameongeza.


Kimario amesema Benki ya NMB inatambua umuhimu wa kubuni na kufanya maboresho zaidi kwenye huduma zake, hususan za kidijitali kwa nia ya kurahisisha huduma kwa wateja wake.

“Tutaendelea kuwa karibu na wateja wetu ili kuishi kaulimbiu yetu ya NMB Karibu Yako,” amesema meneja huo na kuongeza kuwa katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Benki hiyo itaendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii, ili furaha ya wafanyakazi wake pia iende kuwagusa Watanzania wenzao katika maeneo yenye changamoto.

Maadhimisho ya aina hiyo yamefanyika pia katika Benki ya NMB Tawi la Sirari mpakani na nchi ya Kenya, kwa wakati mmoja.


Wateja walioshiriki katika maadhimisho hayo wamepongeza na kuelezea kuridhishwa na huduma nzuri zinazoendelea kutolewa na Benki hiyo.

“Kuna mabadiliko makubwa tunayoona kila tunapokuja kupata huduma, na sasa hivi unaweza kupata huduma za NMB mfano sim banking hata ukiwa nyumbani. Kwa kweli tunafurahi sana na tunawashukuru kwa huduma zenu,” amesema mmoja wa wateja walioshiriki katika hafla ya maadhimisho hayo.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote ameimiminia Benki ya NMB sifa kemkem, akisema ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.


“Mbali na kuboresha huduma, Benki ya NMB inatoa misaada kwa jamii na hivi karibuni tulipokea msaada wa mabati 600 kwa ajili kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule zetu za msingi nne,” Komote amabye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya maadhimisho hayo amesema.

Hafla ya maadhimisho hayo ya Wiki ya Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB pia imefanyika sambamba na baadhi ya wateja kutunukiwa vyeti malumu vya kutambua mchango wao kwa maendeleo ya Benki hiyo, wakiwemo wafanyabiashara Range Boaz Range na Mwita Chacha Nyamete.


1 comment:

  1. Video slots are a computerized model of a standard slot machine. The fundamentals of the sport are just the same, nonetheless when you play video slots you would possibly discover that the games offer extra features similar to bonus rounds, wilds and scatter symbols. Free video slots are also in style amongst gamers looking to perfect their expertise, hone a brand new} technique or learn all there is be} to learn about a brand new} title. Whether you’re wondering if a brand new} game is value your money, or you’re looking to discover 우리카지노 out the secret to profitable a difficult bonus round, free video slot games are the way way|the means in which} to go.

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages