NEWS

Monday 3 October 2022

Uchaguzi CCM: Ngicho ashinda kwa kishindo Tarime, Ongujo acheka Rorya, Begha ashindwa kutetea Serengeti


Marwa Daudi Kebohi (Ngicho)

Na Mara Online News
-------------------------------

MWANASIASA Marwa Daudi Kehohi (Ngicho), amefanikiwa kutetea kwa kishindo nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime mkoani Mara, katika uchaguzi uliofanyika usiku wa kumkia leo.

Habari za hivi punde zinasema Ngicho ameshinda baada ya kuvuna kura 777, akimwacha mbali mshindani wake wa karibu, Nyerere Jackson Mwera aliyepata kura 269, huku Marwa Mairo akishika mkia katika kinyang'anyiro hicho kwa kuambulia kura 10.

“Uchaguzi umeenda vizuri na Marwa Daudi Kehobi (Ngicho) ameshinda kwa kura 777, amefuatiwa na Nyerere Jackson Mwera ambaye amepata kura 269 na watatu ni Mairo ambaye amepata kura 10,” Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Valentine Maganga ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu kutoka ukumbi wa TTC akiwa katika hitimisho la uchaguzi huo.

Kwingineko katika wilaya ya Rorya, mwanachama Ongujo Wakibara Nyamarwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Rorya.

Ongujo Wakibara Nyamarwa

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana usiku, Ongujo ameshinda kwa kura 708, akifutiwa na Zephania Ombuo aliyepata kura 232 na Hamis Marandi (kura 8).

Kutoka Musoma, Mathias Marwa anaripoti kuwa Benedictor Magiri naye amefanikiwa kutetea nafasi ya Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma, kwa kupata kura 280 ya Daudi Misango (kura 247).

Habari nyingine zinasema Mrobanda Japan Mkome amechguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Serengeti, akiwashinda wapinzani wake katika uchaguzi huo, akiwemo Jcob Begha Gehamba aliyekuwa akitetea nafasi hiyo.
Jacob Begha Gehamba

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages