NEWS

Sunday, 2 October 2022

Chonchorio ang’ara Ujumbe Mkutano Mkuu CCM Taifa, Mwangwa naye acheka, Bwire Mageuzi abwagwa


Daniel Chonchorio (Chox)

Na Mara Online News
------------------------------

MWANASIASA kijana Daniel Chonchorio (Chox), amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, katika uchaguzi uliofanyika jana usiku.

"Katika nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Chonchorio ndiye anaongoza kwa kura nyingi," Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Valentine Maganga ameiambia Mara Online News asubuhi hii kwa njia simu kutoka ndani ya kikao cha kuhitimisha uchaguzi huo.

Wajumbe wa mkutano huo pia wamewachagua Francis Chacha (Mwangwa) na Manchare Heche, kuwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Francis Chacha (Mwangwa)

Manchare Heche

Miongoni mwa wanasiasa wakongwe waliobwagwa katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindani mkali kuwahi kushuhudiwa, ni James Bwire (Mageuzi), aliyewahi kuwa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwnza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages