NEWS

Saturday 1 October 2022

Upepo wa Chonchorio kinyang’anyiro cha Mjumbe Mkutano Mkuu CCM Taifa usipime


Daniel Chonchorio (Chox)

Na Mara Online News
------------------------------

MGOMBEA nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chonchorio (Chox), ametajwa kuwa na mvuto na ushawishi mkubwa kwa wajumbe kuelekea uchaguzi wenyewe.

Wajumbe waliozungumza na Mara Online News kwa nyakati tofauti mjini Tarime leo Oktoba 1, 2022, wanamuelezea Chonchorio kama sura mpya kwenye kinyang’anyiro hicho, inayoweza kuwa chachu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi ndani na nje ya CCM.

“Kwanza huyu kijana ni mfanyabiashara na mwekezaji mzawa, na sasa hivi amejenga kiwanda cha kusindika alizeti - ambacho kitakuwa mkombozi kwa wakulima, siyo tu kwa Tarime bali Kanda ya Ziwa nzima,” amesema mwana-CCM ambaye ni mjumbe wa uchaguzi huo.

Mjumbe mwingine amesema “Wajumbe wengi tuna imani kwamba kijana huyu atakuwa msaada mkubwa kwa chama na wananchi kwa ujumla. Njia yake ni nyeupe kabisa katika uchaguzi huu.”

Katika kinyang’anyiro hicho cha Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Chonchorio anachuana na makada wengine kadhaa, akiwemo Joyce Ryoba Mang’o.

Uchaguzi huo utafanyika kesho Oktoba 2, 2022 huku mchuano ukitarajiwa kuwa mkali kuwahi kushuhudiwa - kama inavyotarajiwa pia kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, ambapo Marwa Daudi Kebohi (Ngicho) anatetea wadhifa huo.

Marwa Daudi Kebohi (Ngicho)

Joyce Ryoba Mang'o

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages