NEWS

Monday 14 November 2022

Prof Muhongo kusafirisha wajumbe chaguzi za viongozi CCM Mara


Prof Sospeter Muhongo

Na Mara Online News
----------------------------------

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amekubali kuchangia usafiri wa wajumbe wa chaguzi za viongozi wa CCM ngazi ya mkoa wa Mara.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mbunge huyo kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa wajumbe hao watasafirishwa kutoka Musoma Vijijini kwenda Musoma Mjini na kurudishwa.

Chaguzi zitakazofanyika mwezi huu ni za viongozi wa Jumuiya za UVCCM, Wazazi na UWT, kisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages