Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT, Rhobi Samwelly.
Na Mwandishi Wetu, Musoma
--------------------------------------------
WANAWAKE wameng'ara katika chaguzi za viongozi wa nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara.
Makada hao wa CCM ni pamoja na mtetezi wa haki za watoto wa kike na wanawake, Rhobi Samwelly, amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT kutokea mkoa wa Mara.
Rhobi alivuna kura 411 huku washindani wake [wa pili na wa tatu] wakigawana kura 37 katika uchaguzi uliofanyika mjini Musoma, juzi.
Hii ni Mara ya pili kwa Rhobi kuchaguliwa kushika wadhifa huo ndani ya chama hicho tawala.
Wengine waliong’ara katika chaguzi za CCM ni Nancy Msafiri aliyeibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara, Nancy Msafiri.
Naye Mwanadada Mary Daniel alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM Mkoa wa Mara baada ya kuwatimulia vumbi washindani wake; James Ibanga na Baraka Magira.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Daniel.
Kwa upande mwingine, Mgore Miraji Kigera alishinda nafasi ya Ujumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa kutokea Mkoa wa Mara.
No comments:
Post a Comment