NEWS

Saturday 3 December 2022

Barrick yatoa taarifa ya tukio la uvamizi mgodi wa North Mara



Na Mara Online News
-----------------------------------

KAMPUNI ya Barrick imetoa taarifa ya tukio la uvamizi katika mgodi wake wa dhahabu wa North Mara lililotokea usiku wa Novemba 30, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kampuni hiyo kwa lugha ya Kiingereza leo Desemba 3, 2022, kundi la watu zaidi ya 100 wakiwa na mapanga na mikuki - maarufu kwa jina la intruders, walijaribu kuruka ukuta na 70 miongoni mwao waliweza kuingia na kuanza kupora mali za mgodi huo.

Taarifa hiyo inasema walinzi wa kampuni binafsi wasio na silaha walijaribu kuzuia uvamizi huo lakini walizidiwa nguvu huku wakishambuliwa na kundi hilo.

Baada ya kuona hivyo, mgodi wa North Mara uliomba msaada kutoka kwa askari wa Jeshi la Polisi ambao walifika na kutumia muda wa saa moja na nusu kuwaondoa wavamizi hao mgodini, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa wakati wa operesheni hiyo mmoja wa wavamizi alijeruhiwa na polisi walimsafirisha kwenda kupata matibbu kwenye hospitli iliyo jirani, ambapo kwa bahati mbaya alifariki dunia, pengine kutokana na majeraha aliyopata.

Mara Online News inaendelea na juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime-Rorya kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages