NEWS

Thursday 1 December 2022

Barrick North Mara yang’arisha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani katika wilaya ya Tarime



Na Mwandishi Wetu, Tarime
------------------------------------------

KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Barrick kupitia mgodi wake wa dhahabu wa North Mara imeratibu na kufadhili shughuli mbalimbali za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Maadhimisho hayo ambayo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali yamefanyika kiwilaya katika viwanja vya halmashauri hiyo vilivyopo Nyamwaga leo Desemba 1, 2022.


Barrick imewezesha kufanyika kwa maadhimisho ya siku hiyo ya Ukimwi kwa kushirikiana na wadau wake; RIN Co. Ltd, AKO Group Ltd na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini).

Akihutubia wananchi baada ya kukagua mabada ya huduma tofauti za afya zilizotolewa wakati wa maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele ameishukuru na kuipongeza Barrick North Mara kwa maandalizi mazuri na huduma mbalimbali.

Kanali Mntenjele akihutubia wananchi katika maadhimisho hayo

Aidha, Kanali Mntenjele amewahimiza wananchi wote kufahamu kuwa Ukimwi bado na hivyo kuendelea kuchukua tahadhari na kupima afya ili kujua hali zao.

“Ukimwi bado upo tuendelee kuchukua tahadhari, kupima afya zetu na kuzingatia masharti ya kitaalamu,” amesema Kanali Mntenjele.


Mkuu huyo wa wilaya pia amepata fursa ya kukabicdhi Barrick North Mara na wadau wengine vyeti maalumu vya kutambua michango yao ya hali na mali iliyosaidia kufanikisha maadhimisho hayo.

Dkt Nicholaus Mboya kutoka Barrick North Mara akipokea cheti cha kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha maadhimisho hayo.

Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu North Mara, Dkt Nicholaus Mboya ambaye ni Mratibu wa Afya wa mgodi huo, naye amewashukuru wadau wote waliosaidiana katika kufanikisha maadhimisho hayo.

Awali, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Dkt Joseph Mziba amesema maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) katika halmashauri hiyo yamepungua kutoa asilimia 2 mwaka 2022 hadi asilimia 1.8 mwaka huu [2022].

Hata hivyo Dkt Mziba amesema halmashauri hiyo inaendelea kueneza kwa wananchi elimu, tiba kinga na kugawa condom kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya VVU.

Kikundi cha ngoma ya asili cha Nyakitari ni miongoni mwa vikundi vya wasanii vilivyotumbuiza katika maadhimisho hayo

Kulikuwepo pia na shuhuda wa Ukimwi anayeishi na VVU ambaye ametoa wito kwa wananchi akisema “Jitokezeni kupima VVU ili muweze kuishi kwa kujiamini wala siyo kwa matumaini.”

Taasisi ya NYP+ nayo iliungana na Barrick na wadau wengine kutoa huduma mbalimbali za afya bure kwa wananchi, zikiwemo za ushauri nasahaha, kupima VVU, kifua kikuu, saratani ya mlango wa shingo ya uzazi, sickle cell, ini, uchangiaji damu salama na chanzo za UVICO-19 na polio.


Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu inasema "Zingatia Usawa, Tokomeza VVU. Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko."

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages