Rais Dkt Samia Suluhu Hassan |
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
-----------------------------------------------
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amefengua Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na kusema ilani ya chama hicho inatekelezwa kwa kasi kubwa ili kuleta maguezi makubwa ya maendeleo ya kisekta nchini.
“Kwa kweli kazi ya utekelezaji wa ilani unaenda kwa kazi kubwa sana,” Rais Dkt Samia ambaye pia ni Mwenyekitii wa CCM Taifa amesema katika sehemu ya hotuba yake ya ufunguzi wa mkutno huo unaofanyika leo Desemba 7, 2022 jijini Dodoma.
Aidha, kiongozi huyo wa nchi amesema mageuzi makubwa yanaendelea kukirudisha chama hicho tawala kwa wananchi na amewataka viongozi wapya waliochaguliwa kuhakikisha kinaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa siasa za kistaarabu na uongozi bora.
No comments:
Post a Comment