NEWS

Wednesday 7 December 2022

Naibu Waziri Sagini na vigogo wengine wagalagazwa UNEC, Wassira ang’ara


Jumanne Sagini

Na Mara Online News
-----------------------------------

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ni miongoni mwa vigogo kadhaa waliobwagwa katika kinyang’anyiro cha Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara.

Sagini ambaye pia ni Mbunge wa Butiama mkoani Mara, na vigogo wengine walishindwa kuchomoza katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindni mkali kwenye Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM Taifa uliofanyika jijini Dodoma jana Desemba 7, 2022.

Baadhi ya vigogo wengine walioshindwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Hata hivyo mawaziri wengi, wakiwemo Dkt Angeline Mabula (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angela Kairuki (TAMISEMI) na January Makamba (Nishati) walipenya katika kinyang’anyiro hicho.

Naye mwanasiasa maarufu, Stephen Masato Wassira ambaye alipata kuwa waziri katika wizara mbalimbali nchini na mbunge wa Bunda mkoani Mara, ni miongoni mwa wagombea waliong’ara katika kinyang’anyiro hicho.
Stephen Masato Wassira

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages