NEWS

Thursday 1 December 2022

Shule za Moregas ya Tarime na Leaders ya Rorya zafungiwa kwa udanganyifu wa mtihani wa darasa la saba



Na Mara Online News
------------------------------------

SHULE mbili za mkoani Mara, ni miongoni mwa shule 24 ambazo vituo vyake vya mitahani vimefungiwa na Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA) baada ya kuthibika kufanya udanganyifu katika Mtihani wa Kitaifa wa darasa la saba uliofanyika mwaka huu (2022).

Shule hizo ni Moregas Primay iliyopo Sirari katika Halmahauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) na Leaders Primary ya wilayani Rorya, Mara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athuman Amasi (pichani juu), jijini Dar es Salaam leo, shule nyingine zilizokumbwa na adhabu hiyo ni Kadama (Chato), Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro (Arusha), Sahare (Tanga), St. Anne Marie (Ubungo) na Ukerewe Primary iliyopo Mwanza.

Nyingine ni Peaceland (Ukerewe), Karume (Bukoba), Al Hikma Primay (Dar es Salaam), Kazoba (Karagwe), Mugini (Magu - Mwanza), Busara (Magu - Mwanza), Jamia (Bukoba), Winners na Musabe za jijini Mwanza.

Shule nyingine kwenye orodha hiyo ni Elisabene (Tunduma), High Challenge (Arusha), Tumaini (Sengerema), Olele (Mwanza), Must Lead (Chalinze), Kivulini (Mwanza) na St. Severin ya Biharamuro.

Wakati huo huo, NECTA imefuta matokeo yote ya watahiniwa 2,194 sawa na asilimia 0.16 ya watahaniwa 1,350,881 waliofanya mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages