NEWS

Monday 6 February 2023

Mwaka wa fedha 2023/2024: Madiwani Halmashauri Tarime Mji wapitisha bajeti ya Sh bilioni 26.7



Na Mara Online News
-----------------------------------

MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, wameidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya halmashauri hiyo - kiasi cha shilingi bilioni 26.711 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Wamepitisha bajeti hiyo katika kikao cha baraza lao kilichofanyika kwenye ukumbi wa jengo jipya la utawala la halmashauri hiyo - kilichoongozwa na Mwenyekiti, Daniel Komote, leo Februari 6, 2023.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji waa Tarime, Daniel Komote akizungumza kikaoni

Awali, akisoma mpango huo wa bajeti, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri hiyo, Victor Magafu amesema kati ya kiasi hicho cha fedha, shilingi bilioni 7.543 sawa na asilimia 28 ni kwa ajili ya kugharimia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

Shilingi bilioni 15.187 sawa na asilimia 56 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa halmashauri hiyo, amesema Magafu - akitaja vyanzo vya mapato yote hayo kuwa ni Serikali Kuu, makusanyo ya ndani na wahisani mbalimbali.

Amebainisha kuwa makadirio ya bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2023/2024, ina ongezeko la asilimia 1.6 ukilinganisha na bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka wa fedha uliopita [2022/2023] - kiasi cha shilingi bilioni 26.301.

“Ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa vyanzo vipya vya mapato kama vile soko la kisasa na kupandishwa kiwango cha kodi kwa baadhi ya vyanzo vya ndani,” Magafu amefafanua.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages