NEWS

Monday 20 March 2023

Maganya: CCM na Serikali tunawatambua na kuwathamini bodaboda, kazi zao si laana, tutaendelea kuwaunga mkono



Na Mara Online News
-----------------------------------

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya (pichani kushoto), amesema chama hicho tawala na Serikali yake vinatambua na kuthamini kazi ya usafirishaji wa abiria kwa pikipiki (bodaboda) kama zilivyo ajira nyingine za kujipatia kipato.

Maganya ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, ametoa kauli hiyo hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa wananchi kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma leo.

“Tunawatambua, tunawathamini, tunawaenzi na tutaendelea kuwapa support (kuwaunga mkono). Sisi Chama Cha Mapinduzi na Serikali tunajua mnaofanya kazi ya usafirishaji kwa jina maarufu la bodaboda si kazi ya laana… sisi tunajua kazi mnayofanya, umuhimu wake katika jamii, mnaendesha familia zenu, hizi ni ajira kama zilivyo ajira zingine,” amesisitiza kiongozi huyo.

Awali, Maganya alipowasili mkoani Mara kwa ziara hiyo ya kikazi, amepokewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (pichani kulia), ambapo ameanza kwa kuzindua mashindano ya mbio za pikipiki.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages