Na Mara Online News
----------------------------------
CHAMA cha Wanafunzi wa Shule za Sekondari wa Kisabato (ASSA) Kanda ya Tarime Kati wamepata msaada wa shilingi 750,000 na ahadi ya kompyuta moja kutoka kwa kijana Nyahiri Michael Kembaki.
Nyahiri alitoa misaada hiyo wakati wa mahafali ya kuwaaga wana-ASSA wanaohitimu kidato cha sita, yaliyofanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Tarime Kati, jana Machi 5, 2023.
Nyahiri akizungumza katika mahafali hayo
Nyahiri ambaye naye ni mwana-ASSA alifafanua kuwa fedha alizotoa, pamoja na mambo mengine zitasidia kununua vifaa vya upishi, huku akishauri kompyuta atakayotoa ielekezwe kwa wana-ASSA Tawi la Shule ya Sekondari Tarime.
Wana-ASSA wanaohitimu kidato cha sita wakiimba wimbo wakati wa mahafali yao
Nyahiri aliwapongeza wana-ASSA kutoka matawi ya Shule za Sekondari Ingwe, Manga na Tarime waliohudhuria mahafali hayo.
Mwenyekiti wa ASSA Kanda ya Tarime Kati na Tawi la Shule ya Sekondari Tarime, Philipo Iteremi alimshukuru Nyahiri kwa misaada hiyo, huku akiweka wazi kuwa bado wana uhitaji wa vyombo vya muziki, vikiwemo vinanda viwili na spika tatu kwa ajili ya kufanikisha utume wa Waadventista Wasabto.
Wazazi na walezi wakifuatilia matukio ya mahafali hayo
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi
No comments:
Post a Comment