NEWS

Wednesday 19 April 2023

CCM Tarime wataka dampo la Starehe lihamishwe kuondolea wananchi keroNa Mara Online News
-----------------------------------

KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime mkoani Mara imeiomba Serikali kuhamisha dampo la uchafu lililopo mtaa wa Starehe katani Nyamisangura ili kuwaondolea wananchi kero.

“Tunaiomba Serikali ilifunge dampo hili na kulihamishia kwingine kwani limekuwa kero kwa wakazi wa eneo hili,” amesema Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho aliyeoongoza kamati hiyo kutembelea eneo hilo leo Jumatano Aprili 19, 2023.

Awali, Diwani wa Kata ya Nyamisangura, Thobias Ghati ameieleza kamati hiyo kuwa dampo hilo limekuwa kero ya muda mrefu kwa wakazi wa mitaa ya Starehe na Mwangaza kutokana na uchafu na harufu mbaya.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele amewapa pole wakazi wa maeneo hayo na kuahidi kuwa Serikali itahamisha dampo hilo haraka iwezekanavyo.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages