NEWS

Saturday, 26 August 2023

IAWP yaleta matokeo chanya Jeshi la Polisi Tarime Rorya




Na ASP Minja, Tarime Rorya
--------------------------------------
 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Tarime Rorya limefurahishwa na matokeo chanya ya maofisa wake walioshiriki Mkutano wa Nne wa Mafunzo wa Jumuiya ya Askari Polisi wa Kike Duniani (IAWP) Kanda ya Afrika 2023, yaliyofanyika mwisho mwa Julai mwaka huu jijini Dar es salaam. 

Mwenyekiti wa TPF-net Kanda Maalum ya Tarime Rorya, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Mbunja Matibu amesema askari hao wameonesha kwa vitendo namna ya kutanzua uhalifu, hususan ule unaovuka mipaka. 

SSP Matibu amebainisha kuwa askari hao wajifunza namna ya kukabiliana na uhalifu huo pamoja na kughushi nyaraka na ushiriki wa askari wa kike katika kulinda amani kwenye mataifa yenye changamoto za kiusalama. 


Ameongeza kuwa tangu walipohitimu mafunzo hayo, askari hao wameonesha mabadiliko katika kupambana na uhalifu unaovuka mpaka, huku akibainisha kuwa Mkoa wa Polisi Tarime Rorya ni mmoja ya mikoa ya mipakani mwa Tanzania ambapo wamekuwa wakitoa huduma. 

Pamoja na hayo, askari hao wamehimizwa kuwa mabalozi wazuri katika maeneo wanakofanyia kazi, ikiwemo kuwaelekeza askari wenzao yale waliyofundishwa ili kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao wa kila siku. 

Jumla ya askari 40 kutoka wilaya za kipolisi sita zinazounda Mkoa wa Polisi Tarime Tarime walihudhuria na kupata mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages