
Na Mwandishi Maalumu
---------------------------------



#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi
---------------------------------
KAMPUNI ya Kemanyanki imeandaa mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la 'Kemanyanki Cup' yanayoshirikisha timu 12 za vijana kutoka vijiji 11 vinavyozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, unaoendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
Mashindano hayo yalizinduliwa juzi kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Ingwe iliyopo mji wa Nyamongo, kilomita chache kutoka mgodi wa North Mara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Diwani wa Kata ya Nyamwaga, Mwita Magige.

Diwani Magige (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kemanyanki, Nicolaus Mgaya alisema mashindano hayo yatakuwa fursa kwa vijana kukutana na kubadilishana mawazo ambayo yanaweza kuwa na faida katika maisha yao na jamii inayozunguka mgodi huo.
Yatafanyika kwa kipindi cha wiki mbili, ambapo mechi ya fainali itachezwa Septemba 2, 2023, na kwa mujibu wa Mgaya, washindi; yaani wa kwanza hadi wa tatu watapewa zawadi nono zikiwemo fedha taslimu, lakini pia kila timu itaondoka na zawadi ya jezi za michezo.

“Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi laki saba, mshindi wa pili lakini nne na mshindi wa tatu shilingi laki tatu,” Mgaya alifafanua.
Kemanyanki ni moja ya kampuni za wazawa zinazofanya kazi na Kampuni ya Barrick katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa kutoa huduma mbalimbali.
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi
No comments:
Post a Comment