NEWS

Wednesday 16 August 2023

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngongoro yatoa tamko kujeruhiwa kwa waandishi wa habari
Na Mwandishi Wetu
-------------------------- 

MAMLAKA ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema inashirikiana na Jeshi la Polisi kuwasaka vijana wa Kimaasai waliohusika katika tukio la kuwajeruhi waandishi wa habari na watumishi wa serikali ndani ya hifadhi hiyo. 

“…Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” ilisema sehemu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na NCAA jana jioni, ikieleza kuwa timu hiyo ilikumbwa na mkasa huo wakati ikiwa katika utoaji elimu kwa wananchi waliojitokeza kujiandikisha kuhama kwa hiari katika kijiji cha Endulen kilichopo hifadhini humo. 

“Zoezi la utoaji elimu lilipokuwa likiendelea, vijana wa Kimaasai wakiwa na silaha mbalimbali za jadi, waliwavamia, kuwashambulia na kuwajeruhi kwa silaha. 

“Mamlaka imesikitishwa na kitendo hicho na inatoa pole kwa wote waliojeruhiwa,” ilisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Joyce Mgaya, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kwa Umma wa NCAA. 

Waandishi wa habari na watumishi wa serikali waliojeruhiwa katika tukio hilo walipelekwa kupata matibabu ya dharura katika Hospitali ya FAME Medical iliyopo Karatu, kulingana na taarifa hiyo. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages