NEWS

Tuesday 22 August 2023

Rais Samia ahakikishia Watanzania hakuna atakaeigawa nchiRais Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika Makumira mkoani Arusha, jana.
-----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Arusha
--------------------------------------
 

RAIS Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa la Tanzania. 

“Niliamua kunyamaza kimya na naendelea kunyamaza kimya, nachotaka kuwahakikishia, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa hili,” amesema Rais Samia. 

Aliyasema hayo katika hotuba yake kwenye maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika Makumira mkoani Arusha, jana. 

Kadhalika, Mkuu huyo wa nchi aliwahakikishia Watanzania kuwa “Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye Taifa hili, sasa hayo itoshe kuwa ni ujumbe wangu kwenu.” 

Awali, akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Samia, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt Fredrick Shoo alimpongeza kiongozi huyo wa nchi kwa kuwa kimya dhidi ya kauli kutoka taasisi na wananchi mbalimbali wanaokosoa makubaliano ya uwekezaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai. 

“Nashukuru Mungu amekujaalia hekima kama mama na kiongozi umekaa kimya, lakini kimya chako hicho sio kwamba hufanyii kazi, mimi nasema jambo hili linahitaji hekima kubwa na sisi tunakuombea kwa Mungu ili heshima yote itumike jambo hili muafaka upatikane,” alisema kiongozi huyo wa kiroho. 

Askofu Shoo alisema kanisa hilo linaunga mkono uwekezaji, na kwamba halipingi mkataba huo kwani halina shaka na nia ya Rais Samia kuhusu uwekezaji. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages