NEWS

Monday 14 August 2023

Uongozi wa Chandi wawavutia wazee wa mila kutoka koo 12, wamkabidhi mkuki na ngaoMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (wa pili kushoto) akipokea mkuki, ngao na kigoda kutoka kwa wazee wa koo 12 za kabila la Wakurya wilayani Tarime waliomtembelea nyumbani kwake Mugumu, Serengeti jana.
----------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Serengeti
------------------------------------------

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi amepata baraka za wazee wa mila kutoka koo 12 zinazounda kabila la Wakurya wilayani Tarime. 

Katika tukio hilo la kihistoria, wazee hao ambao walimtembelea Chandi nyumbani kwake Mugumu, wilayani Serengeti jana, walimkabidhi mkuki, ngao na kigoda - ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa kiongozi mahiri wa jamii. 

Walimpongeza Mwenyekiti huyo kwa uongozi uliotukuka na kumuahidi ushirikiano wa dhati katika shughuli za utekelezaji wa Ilani ya chama hicho tawala. 

Ziara hiyo iliratibiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM Kata ya Nkende wilayani Tarime ikiongozwa na Katibu wake, Justin Manga. 
Chandi (wa pili kutoka kulia mbele) akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho Kata ya Nkende, Justin Manga wakati viongozi wa jumuiya hiyo walipomtembelea nyumbani kwake Mugumu, Serengeti. Wa kwanza kulia ni mke wa Chandi, Getruda. (Picha zote na Godfrey Marwa)

Akizungumza baada ya kupokea vitu hivyo, Chandi aliwashukuru wazee hao akisema wamemuongezea nguvu ya kutekeleza majukumu yake ya uongozi kwa uadilifu mkubwa na bila woga, kwa maendeleo ya wana-Mara na taifa kwa ujumla. 

Aidha, naye aliahidi kushirikiana nao bega kwa bega katika kila jambo la kimaendeleo watakalomshirikisha.

Chanzo: SAUTI YA MARA 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages