WATU 93 wamethibitishwa kufariki dunia katika moto ya Maui ulioteketeza mji wa kihistoria wa Lahaina, ikiwa ni ajali mbaya zaidi ya moto nchini Marekani katika karne moja.
“Idadi ya waathiriwa inaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa,” Gavana wa Hawaii, Josh Green alisema jana Jumamosi, huku kazi ya uchunguzi ikiendelea kuwatambua.
Mamia hawajulikani waliko huku wengine wakiyajaza makazi katika eneo la Maui baada ya kuukimbia moto huo.
“Ni siku ngumu. Moto huo hakika utakuwa janga baya zaidi la asili kuwahi kukumba Hawaii,” alisema Green.
“Tunaweza tu kusubiri na kusaidia wale wanaoishi. Lengo letu sasa ni kuwaunganisha watu tunapoweza na kuwapatia makazi na huduma za afya, na kisha kugeukia kujenga upya,” aliongeza.
Wakati moto wa nyika kwa sasa umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa, juhudi za kuuzima kabisa zinaendelea katika sehemu za kisiwa hicho, ikiwa ni pamoja na karibu na mji wa Lahaina, ambao umeharibiwa. BBC
No comments:
Post a Comment