NEWS

Saturday 2 September 2023

Rais Samia amvua Dkt Slaa hadhi ya Ubalozi aliyokuwa nayo tangu mwaka 2017Dkt Wilbroad Peter Slaa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemvua Dkt Wilbroad Peter Slaa hadhi ya Ubalozi kuanzia Septemba 1, 2023, imesema taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kwa vyombo vya habari jana Ijumaa.

Dkt Slaa aliteuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dkt John Pombe Magufuli (kwa sasa ni marehemu) kuwa Balozi Novemba 23, 2017 na baadaye mwaka 2018 alimteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden - nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 2021.

Dkt Slaa aliyewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alipata pia kuwa Mbunge wa Jimbo la Karatu kati ya mwaka 1995 na 2010 kwa tiketi ya chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages