NEWS

Monday, 29 January 2024

Rais Samia kukabidhi zana za uvuvi kwa wavuvi Kanda ya Ziwa kesho



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
---------------------------------------------

NA MWANDISHI WETU, Mwanza
-----------------------------------------------

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kukabidhi zana za uvuvi kwa vikundi vya wavuvi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kesho Jumanne.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla, Rais Samia anatarajiwa kuwasili jijini hapa leo Jumatatu kwa ziara ya kikazi, hususan ya kukabidhi zana za uvuvi.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita, RC Makalla alitoa wito wa kuhimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais katika Uwanja wa Ndege Mwanza.

Alisema maandalizi yalikuwa yamekamilika na kwamba hafla ya kukabidhi zana za uvuvi itafanyika katika uwanja wa Nyamagana.

Kiongozi huyo wa mkoa aliweka wazi kuwa hatua hiyo imeratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, lengo likiwa ni kuwezesha wavuvi kuondokana na zana duni na zilizopitwa na wakati.
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages