NEWS

Tuesday 13 February 2024

Balozi na Waziri Mstaafu Dkt Kamala afariki duniaBALOZI Mstaafu na Waziri wa zamani wa Afrika Mashariki, Dkt. Deodorus Buberwa Kamala (pichani), amefariki dunia.

Taarifa zinasema Dkt Kamala alifariki jana Jumatatu jijini Dar es Salaam.

Dkt Kamala amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera kati ya mwaka 2000 hadi 2010.

Mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri wa wizara hiyo mwaka 2008 hadi 2010.

Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Uholanzi, ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 aliporejea kuwa Mbunge wa Nkenge hadi mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages