NEWS

Thursday 22 February 2024

Chandi atuma salamu za pole kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora



Mwenyekiti wa CCM Mara, Patrick Chandi Marwa (kushoto). Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Tabora, Hassan Wakasuvi enzi za uhai.
------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma
----------------------------------------


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa ametuma salamu za pole, akielezea kupokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho tawala, Hassan Wakasuvi, kilichotokea jana Februari 22, 2024.

“Mwenyekiti wa CCM Tabora ndugu Wakasuvi alikuwa kiongozi mahiri na rafiki yangu wa karibu. Nawapa pole familia ya ndugu Wakasuvi, wanachama wa CCM na wananchi wote wa mkoa wa Tabora kwa msiba huu mkubwa,” amesema Chandi.

Jana Chama Cha Mapinduzi Taifa kilituma salamu za rambirambi, kikisema kitamkumbuka Wakasuvi kwa utii, uaminifu na uzalendo wake katika kukitumikia chama hicho na Taifa kwa ujumla.

“Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt Samia Suluhu Hassan anatoa salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, wanachama wa CCM na Watanzania wote walioguswa na msiba huu,” ilisema sehemu ya salamu za rambirambi zilizosainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages