NEWS

Wednesday 21 February 2024

Dkt Mataragio ateuliwa na Rais Samia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati



Dkt James Peter Mataragio
-----------------------------------


NA MWANDISHI WETU
-------------------------------------


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dkt Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Dkt Mataragio amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tamzania (TPDC).
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages