NEWS

Thursday, 8 February 2024

Madiwani Halmashauri ya Tarime Vijijini waidhinisha makisio ya bajeti bilioni 49/- kwa mwaka 2024/2025, DC Mntenjele ahimiza ushirikiano



Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kilichofanyika Nyamwaga, leo Februari 8, 2024.
----------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News, Tarime
-------------------------------------


BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime [Vijijini] mkoani Mara, limeidhinisha makisio ya bajeti ya mapato na matumizi - kiasi cha shilingi bilioni 49.1 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Hatua hiyo imefikiwa leo Februari 8, 2024 katika kikao cha baraza la madiwani hao kilichofanyika Nyamwaga, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Simion Kiles.


Madiwani kikaoni
--------------------------
Taarifa iliyowasilishwa na Modest Lema kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, imebainisha kuwa fedha hizo zitatokana na mapato ya ndani, ruzuku ya maendeleo kutoka Serikali Kuu na wahisani.

Aidha, imetaja masuala muhimu yaliyozingatiwa katika bajeti hiyo kuwa ni pamoja na Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 - 2025 na vipaumbele vya wananchi ngazi za kata na vijiji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, Mwenyekiti wa Halmashauri, Simion Kiles na Mkurugenzi Mtendaji, Solomoni Shati wamewaomba madiwani kushirikiana na wataalamu katika usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolengwa na bajeti hiyo.

Kikao hicho cha Baraza la Madiwani kimehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Mwl Saul Mwaisenye na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, miongoni mwa viongozi wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages