NEWS

Saturday 10 February 2024

Rais Samia, CCM watuma salamu za rambirambi kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu LowassaEdward Lowassa enzi za uhai
-------------------------------------------

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi, akieleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, kilichotokea leo Februari 10, 2024 jijini Dar es Salaam.

Katika ukurasa wake maalumu kwenye mtandao wa kijamii, Rais Samia ameandika: 

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa. Mheshimiwa Lowassa ameitumikia nchi yetu katika nafasi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 35, akianzia ushiriki wake katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge, Waziri katika wizara mbalimbali na Waziri Mkuu.

"Tumempoteza kiongozi mahiri, aliyejituma na kujitoa kwa nchi yetu. Natoa pole kwa mjane, Mama Regina Lowassa, watoto (Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa na wadogo zako), ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mzito.

"Katika mawasiliano yangu na familia, nimewaeleza kuwa kama taifa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu, na kamwe wasiache kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutafakari neno lake, hasa Kitabu cha Ayubu 1:21.

"Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina."


Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
------------------------------------------

Nacho chama tawala - Chama Cha mapinduzi (CCM) kimetuma salamu za rambirambi kama ifuatavyo:

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages