Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi (mwenye koti) amewasili wilayani Rorya mapema leo Jumanne kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumza na wananchi, ikiwa ni siku chache baada ya kufanya ziara kama hiyo wilayani Serengeti.
Amepokewa na Mkuu wa Wilaya, Juma Chikoka (mwenye suti ya bluu mbele) na viongozi wa chama tawala - CCM. Rorya ni miongoni mwa wilaya za mkoani Mara zinazopakana na Ziwa Victoria.
No comments:
Post a Comment