NEWS

Tuesday 4 June 2024

Chang'e-6:Chombo cha Anga cha China chaanza safari kurejea duniani kutoka mwezini.


 
Chombo cha Anga cha China, Chang'e-6: Safari ya Kurudi Duniani
-----------------------

China inasema chomo chake kimeanza kuondoka upande wa mbali wa mwezi kurejea Duniani kikiwa kimebeba sampuli za kwanza kabisa zilizokusanywa kutoka eneo hilo.

Vyombo vya habari vya serikali vinasema sehemu ya chombo cha Chang'e-6, iliyopewa jina la mungu wa kike wa mwezi katika elimu ya mambo ya asili ya Kichina, kilifanikiwa kuondoka salama kuanza safari ya kurejea mnamo saa 07:38 asubuhi leo Jumanne

Chombo hicho kilitua Jumapili karibu na ncha ya kusini ya mwezi katika hafla ya kwanza ya ulimwengu iliyoadhimishwa na jumuiya ya kimataifa ya sayansi.

China ndio nchi pekee iliyotua upande wa mbali wa mwezi, baada ya kufanya hivyo hapo awali mnamo 2019.

Utawala wa Kitaifa wa Anga za Juu wa China umeita tukio hilo ''jambo lisilokuwa la kawaida katika uchunguzi wa mwezi na binadamu''.

Upande huo wa mwezi - ambao daima hutazamana mbali na Dunia - ni changamoto kufikia kutokana na ardhi yake na mashimo ya kina kirefu.

Ujumbe wa China unalenga kuwa wa kwanza kurejesha sampuli za mawe na udongo kutoka eneo hilo, ambazo wanasayansi wanasema zinaweza kuwa tofauti sana na miamba iliyo karibu na mwezi.

Vyombo vya habari vya serikali vilichapisha video kutoka sehemu ya anga za juu ya China zikionyesha chombo husika kikipeperusha bendera ya China baada ya kukusanya sampuli hizo za thamani.

China yaweka bendera juu ya uso wa mwezi kabla ya kurudi kwa Chang'e 6
-------------------
 Je unaamini kwamba kitendo cha China kusafiri na kurudi kutoka mwezini ni hatua muhimu? Hebu tujulishe mawazo yako kuhusu kile unachohisi kuhusu tukio hili la kushangaza!
Kutoa maoni yako gusa maneno yaliyopo chini ya Habari hii yakisomeka kama
' SIGN IN WITH GOOGLE'

CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages