NEWS

Saturday 15 June 2024

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee kufanyika kitaifa mkoani Mara leoSehemu ya wazee walioshiriki kongamano lao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda jana Ijumaa
----------------
 
Na Mwandishi Wetu, Bunda
-----------------------------------
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima.

Madhimisho hayo ambayo yanafanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Miembeni wilayani Bunda, yameandaliwa na kuratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la HelpAge Intranational - Tanzania.

Maadhimisho hayo yalianza juzi Alhamisi kwa matukio ya michezo na upimaji afya kwenye viwanja vya Miembeni, na jana Ijumaa lilifanyika kongamano la wazee katika Chuo cha Ualimu Bunda, kisha kutembelea wilayani Butiama nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema: "Utu, Usalama na Ustawi ni Nyenzo ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wazee."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages