NEWS

Friday 14 June 2024

Mara Press Club yaliomba Jeshi la Polisi Mwanza kuweka wazi tuhuma za mwandishi wa habari Dinna

Mwandishi wa habari wa Dimma Online, Dinna Maningo

Na Mwandishi Wetu, Tarime 

...................................................................


Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imeliomba Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuweka wazi tuhuma zinazomkabili mwandishi wa habari wa blogu ya Dima Online, Dinna Maningo.

“Tuna imani Jeshi la Polisi mkoani Mwanza litatoa taarifa kuhusu tuhuma zinazomkabili mwandishi na mwanachama wetu wa Mara Regional Press Club, ndugu yetu Dinna Maningo bila kuchelewa," Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Juni 14, 2024.

Jacob amesema Dinna alikamatwa nyumbani kwake mjini Tarime, Mara jana majira ya saa mbili usiku na hadi leo mchana alikuwa anashikiliwa katika kituo cha polisi Tarime

“Mara tu baada ya kukamatwa kwa Dinna nilipata taarifa na nilifika kituo cha polisi Tarime, tukaonana, alikuwa vizuri lakini aliniambia polisi waliomkamata hawakumwambia sababu ya kumkamata," Jacob amesema kwa kifupi.


Jacob amesema leo Ijumaa pia amefika katika kituo cha polisi Tarime na kuonana na Dinna ambapo amemueleza kuwa askari polisi waliomkamata wamemwambia wanamsafirisha kwenda jijini Mwanza wakati wowote kuanzia sasa.


Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amesema MRPC inawasiliana kwa karibu na uongozi wa Mwanza Press Club ili kusaidiana kufuatilia tukio hilo.

“Tuna imani jeshi letu la polisi litafanya kazi yake kwa weledi ili haki iweze kutendeka kwa ," amesema Jacob.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages