NEWS

Monday 3 June 2024

Waziri wa Mambo ya Ndani atangaza kuvunja mtandao wa ‘intruders’ NyamongoWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, 
Hamad Masauni.
-----------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime
-------------------------------------


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni msako mkali dhidi ya mtandao aliouita mpana wa watu wanaovamia na kuiba mawe ya dhahabu katika mgodi wa North Mara uliopo Nyamongo, wilaya ya Tarime, mkoani Mara.

Alitoa kauli hiyo ya serikali wiki iliyopita, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Murwambe, jirani na mgodi huo.

“Nimeangalia uwezekano wa kukata mnyororo wa watu wanaoshughulika na uvamizi wa mgodi huu, tunajua ni mtandao mpana sana, tuhatakikisha Jeshi la Polisi linawabaini na kuwakamata popote pale walipo.

“Nasikia wako watu huko, wengine wako ndani ya mgodi, wengine mtaani huku, wengine hata hawana sehemu ya kuchimba madini lakini wanauza madini, wanayapata wapi?

“Kwa hiyo sasa hivi maelekezo yetu ni kwamba nguvu ielekezwe kwa hao vinara wanaochochea vijana kwenda kuiba madini ili kukata mzizi, wakamateni wote popote walipo tuuvunje huo mtandao,” alisisitiza Waziri Masauni.

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick Gold kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages