NEWS

Saturday, 13 July 2024

Mkuu wa polisi ajiuzulu Kenya,Raisi Ruto aridhia

Inspecta Jenerali Wa polisi Eng.Japheth N.Koome aliyejiuzulu nchini Kenya
                            -------------

Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya amejiuzulu kufuatia wiki kadhaa za maandamano yenye ghasia ambapo zaidi ya watu 40 waliuawa.

Mashirika ya haki za binadamu yameshutumu polisi kwa kuwapiga risasi makumi ya waandamanaji, baadhi yao kuwaua, na kuwateka nyara au kuwakamata mamia kiholela.

Maandamano yalizuka nchini Kenya katikati ya mwezi uliopita kupinga mapendekezo ya nyongeza ya ushuru. Waandamanaji walivamia bunge muda mfupi baada ya wabunge kupitisha mswada huo tata. Hatua ya Rais William Ruto kuiondoa ilifeli kuzima maandamano. Alivunja baraza la mawaziri siku ya Alhamisi .

Kuna mipango ya kuendelea na maandamano ya kuchochea mageuzi.

"MHE. William Samoei Ruto, Ph.D, CGH, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, tarehe 12 Julai, 2024, amekubali kujiuzulu kwa Eng. Japheth N. Koome, MGH, kama mkuu waPolisi," sehemu ya taarifa hiyo imesema

CHANZO: BBC


Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages