Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,
Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo.
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Wananchi wa vijiji 17 katika jimbo la Musoma Vijijini wameamua kushirikiana katika ujenzi wa zahanati za vijiji hivyo ili kuboresha huduma za afya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi wa mbunge wa jimbo hilo juzi, tayari baadhi ya vijiji hivyo vimeanza kupokea michango ya ujenzi wa zahanati hizo kutoka serikalini.
Zahanati mpya zinajengwa katika vijiji vya Bulinga, Burungu, Butata, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kataryo, Kwikerege, Kurukerege, Kurwaki, Mabuimerafuru, Maneke, Nyabaengere, Nyambono na Nyasaungu
Jimbo la Musoma Vijijini linaongozwa na Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, linaundwa na kata 21 zenye vijiji 68.
Kwa sasa jimbo hilo lina Hospitali mpya ya Halmashauri ya Wilaya, vituo vya afya sita na zahanati 28, kati ya hizo, 24 ni za serikali na nne ni za binafsi.
“Wadau wa maendeleo, wakiwemo wazaliwa wa Musoma Vijijini, wanaombwa kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya vijijini, ukiwemo ujenzi wa zahanati mpya,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya ofisi ya mbunge.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Taasisi ya Nyambari Nyangwine yazinduliwa kwa kishindo Dar, serikali yaahidi kuiunga mkono, wafanyabiashara maarufu kutoka India washiriki
>>Soko Kuu Mwanza kuchochea uchumi wa wafanyabiashara
>>Watu 15 mbaroni kwa kuwashambulia askari wa usalama barabarani wakitekeleza majukumu yao wilayani Serengeti
No comments:
Post a Comment