NEWS

Friday 20 September 2024

Soko Kuu Mwanza kuchochea uchumi wa wafanyabiashara




Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News 
Mwanza

Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amekagua maendeleo ya mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Soko Kuu Mwanza na kueleza kuridhishwa na kiwango cha ubora wa kazi inayoendelea.

Katika ziara hiyo ya Jumanne iliyopita, Waziri Mwigulu alielezwa kwamba mradi huo ambao unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 23.4 zilizotolewa na serikali, umefikia asilimia 96.

Mbali na kupendezesha jiji la Mwanza, ujenzi wa mradi huo ukikamilika utawezesha wafanyabiashara mbalimbali wapatao 1,400 kupata maeneo ya kuendeshea shughuli zao katika maduka 514 na vizimba 705.

Soko hilo linatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara, kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wafanyabiashara katika Kanda ya Ziwa na kuongeza mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 kwa mwaka.

Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages