NEWS

Wednesday, 18 December 2024

Rais Samia amteua Kaji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga.

Kabla ya uteuzi huo, Kaji alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages