NEWS

Thursday, 19 December 2024

Vinicius Jr ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa FIFA



Vinicius Jr

Mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil, Vinicius Jr amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume kwenye Tuzo za FIFA Best Awards.

Vinicius alifanya kazi kubwa katika mechi za Real Madrid na kutwaa Kombe la Champions League na La Liga msimu 2023-2024, akifunga mabao 24 na kutoa pasi za magoli 11.

Katika hafla hiyo, kiungo wa Barcelona, ​​Aitana Bonmati alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka kwa wanawake kwa mwaka wa pili mfululizo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Vinicius kushinda tuzo hiyo. Tuzo za Ballon d'Or na Fifa Best Awards ndizo zenye hadhi kubwa zaidi katika soka.
Kiungo wa kati wa Uhispania na Man City na mshindi wa Euro 2024, Rodrigo Hernández Cascante alimaliza wa pili nyuma ya Vinicius katika tuzo hiyo, huku mchezaji wa Real Madrid, Muingereza Jude Bellingham akishika nafasi ya tatu.
Chanzo: BBC Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages