
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Watu kadhaa wanahofiwa kufa na wengine kujeruhiwa vibaya katika ajali ya basi la Kisire Luxury Coach linalofanya safari kati ya jijini Mwanza na Tarime - Sirari mkoani Mara, iliyotokea jirani na daraja la Magu, Mwanza muda mfupi uliopita leo Desemba 19, 2024.
Mara Online News imewasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa akasema yuko njiani kuelekea eneo la tukio. “Nakaribia eneo la tukio, nikifika nitakupa taarifa,” amesema kwa simu dakika chache zilizopita.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Nyambari, Maswi wabeba harambee ya Kurya Social Group, zaidi ya milioni 20/- zapatikana Namba Tatu akimwakilisha mgeni rasmi
>>Musoma Vijijini: Wazazi CCM wamtunuku Prof Muhongo Tuzo ya ‘Uchaguzi wa Serikali za Mitaa’
>>Mara Press haitafanya kazi na online TV, blogs ambazo hazijasajiliwa TCRA – Mugini
>>TAMISEMI yatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2025
No comments:
Post a Comment