NEWS

Wednesday, 7 May 2025

Rais Samia amteua Twange kuwa bosi mpya wa TANESCO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
----------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam, Lazaro Jacob Twange, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO).

Uteuzi huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam katika taairfa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, kuhusu uhamisho na uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Twange anachukua nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la umma, Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga aliyefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari wilayani Bunda, Mara mwezi uliopita.

Nafasi ya Twange ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo sasa inachukuliwa na Albert Msando, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Taarifa ilieleza kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Mghamba Kubecha, amehamishiwa Hadeni kuziba pengo lililoachwa na Msando.

Naye Dadi Horace Kolimba amehamishwa kutoka Karatu kwenda Tanga, wakati Mkuu mpya wa Wilaya ya Karatu ni Lameck Karanga Nganga.

Katika uteuzi huo, Bahati Migiri Mfungo aliyekuwa Afisa Tarafa ya Mbuguni, wilayani Arumeru amepandishwa cheo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu.

Rais pia amemteua Andrew William Massawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othaman aliyemaliza muda wake.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages