NEWS

Saturday 10 August 2019

ZAIDI YA 60 WAFARIKI KATIKA AJALI YA LORI LA MAFUTA MOROGORO


Na Mwandishi wetu,
  Idadi ya watu waliokufa katika ajali ya gari la mafuta ambayo imetokea Morogoro leo asubuhi  imefikia 62 na majeruhi  zaidi ya 70.
 Majeruhi wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na wengine waliojeruhiwa vibaya wamekimbizwa katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Rais John Magufuli ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wote waliopoteza
jamaa zao katika ajali hiyo mbaya  na kuwaombea majeruhi wapone haraka.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages