NEWS

Sunday 20 October 2019

WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2019 WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI




Na mwandishi wetu,

Jumla watahiniwa 159 wa kidato cha IV 2019 wa shule ya sekondari Nkende iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wamemshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuwapatia elimu bure kwa miaka mine mfululizo.

Wanafunzi  hao wameahidi kufaya vizuri katika mtihani wao ambao unatarajia kuanza mwezi ujao .

“ Kwa sababu sisi ndio wakwanza tunamuahidi  Serikali na Rais wetu  Kuwa tutafanya vizuri katika mithani yetu “, amesema  Faustina Ghati ambaye ni mmoj wa watahiniwa wa kidato cha nne 2019 katika shule hiyo ya Nkende


"Baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakishindwa kufikia ndoto zao kama vile kuwa madaktari  kutokana na ukosefu wa ada,",amesema Rhobi Joseph Thomas ambaye pia ni mtahiniwa katika shule hiyo ya Nkende.




Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Gidion Chacha amesema wanafunzi hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mitihani yao.

Mkuu wa shule ya sekondari ya Nkende Samson Hagai amesema  mpango wa elimu bure umepunga mzigo kwa wazazi .

“ Hata wanafunzi wenye uwezo darasani lakini wanatoka kwenye familia ambazo zilikwa haziwezi kulipa ada sasa wanasoma bila tatizo  na idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari umeongezeka “, amesema Hagai.

Shule hiyo ya Nkende ina wanafunzi zaidi ya 800 ambao wananufaika na mpango wa elimu bure.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages