Neema imerejea Yanga kufuatia kurejea kwa wachezaji wake
watano waliokuwa majeruhi baada ya kuanza mazoezi mepesi juzi Jumatatu.
Wachezaji hao walianza mazoezi wakiwa
katika program maalum wakati kikosi cha timu hiyo kikiwa dimbani kucheza dhidi
ya Friends Rangers ambayo ililala kwa mabao 4-2.
Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana,
Paul Godfrey 'Boxer', Lamine Moro na Sadney Urikhob ndiyo wachezaji waliokuwa wakifanya
mazoezi hayo wakati mechi inaendelea.
Kurejea kwa wachezaji hao kumeanza
kutia morali kwa Yanga ambayo itakabiliana na Pyramids FC katika mchezo wa
Kombe la Shirikisho Afrika Oktoba 27 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment