Taasisi ya African
Youth Empowerment (AYE) Kanda ya Ziwa imeandaa mbio za Marathon ambazo
zitafanyika Mjini Bunda Mkoani Mara
Disemba 12 mwaka huu ambapo mshindi wa wakwanza atazawadiwa shilingi laki mbili.
Mratibu wa AYE Kanda ya
Ziwa Hussein Musa ameiambia Mara Online
News kuwa mbio hizo zitahusisha watoto kuanzia umri wa miaka 10-15, wazee,
watumishi wa serikali na washiriki rasmi wa mbio hizo.
“ Maandalizi ya mbio hizo yanaendelea vizuri na
usajili umeshaanza”, amesema mratibu wa AYE Kanda ya ZIWA.
AYE ni taasisi ambayo
inasadia kuendeleza maisha ya vijana kielimu, kiuchimi na kimichezo .
No comments:
Post a Comment