NEWS

Friday, 23 October 2026

Rais Samia ateua Wenyeviti wapya Bodi za TANAPA, TAWA, TTB

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wapya wa Bodi za taasisi tatu.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imewataja walioteuliwa kuwa ni Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara, Zuhura Sinare Muro na Meja Jenerali Mstaafu Hamis Rajab Semfuko.

Jenerali Mstaafu Waitara ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA).

Zuhura Sinare Muro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Naye Meja Jenerali Mstaafu Semfuko ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages