NEWS

Tuesday 26 November 2019

AGIZO LA MKURUGENZI WA MJI WA TARIME



 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa(kushoto pichani hapo juu) leo Novemba 26,2019 ameagiza  wa watendaji wa kata  kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa  ili kuhakikisha wanafunzi  wote waliofaulu mtahihani wa darasa la saba mwaka huu wanapata nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari mapema mwakani.

Akiongea katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo, Ntiruhungwa amesema wanafunzi 2,000 wanatarajia kijiunga kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za serikali zilizopo katika mji huo wa Tarime.

Amesema upungufu uliopo ni vyumba takribani 15 vya madarasa na kusisitiza kuwa lazima watoto wote waliofaulu wajiunge na elimu ya sekondari ili waweze kunufaika na mpango wa serikali ya awamu ya tano wa elimu bila malipo.

Afisa Elimu Taaluma wa Halmshauri ya Mji wa Tarime Matiko John  akifafanua jambo katika kikao hicho

 Wananchi wa Tarime ni  wasikivu na wastaarabu tushirikiane nao kujenga vyumba vya madarasa na serikali ipo tayari kusaidia ", amesema Ntiruhungwa

Mtendaji wa kata ya Turwa Mzurukwao akichangia hoja katika kikao hicho




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages