Na Mwandishi wetu
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dr Pindi Chana jana
alitembelea kituo cha pamoja cha forodha
cha Holili - Taveta na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha diplomasia ya uchumi
kati mataifa ya Tanzania na Kenya .
Balozi Pindi Chana aliwataka watumishi waliopo
katika mpaka huo kuondoa vikwazo vyote visivyo vya kiforodha yaani non taarif
–barriers.
“ Tujitahidi kuwawezesha wafanyabisahara wa
nchi zetu wanaotumia mpaka wa Holili – Taveta kuondokana kabisa na vikwazo
visivyo vya kiforodha” , aliagiza balozi
Dr Chana.
Dr Pindi Chana
alisema mpaka wa Holili- Taveta ni muhimu katika kusafirisha bidhaa
mbalimbali ikiwemo mazao aina ya vitunguu na mahindi kutoka Tanzania kwenda Mombasa nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment